Lucid tv
Lucid tv
  • 47
  • 527 248
🔴 ROZARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA | THE SEVEN SORROWS OF MARY | SEVEN DOLORS OF MARY
ROSARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Sala ya kwanza
Ee Mungu wangu, nakutolea Rosali hii ya machungu saba ya Bikira Maria kwa ajili ya utukufu wako na kwa heshima ya mama yako Mtakatifu sana. Nitawaza na kushikania naye katika haya aliyopata. Nawe Maria Mama yetu nakuomba, kwa heshima ya machozi uliyomwaga wakati ulipopatwa na machungu haya, utujalie kutubu dhambi zetu. Amina.
Salamu Maria X 3
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA KWANZA (LK 2:25-35)
Katika uchungu wa kwanza tunakumbuka wakati mzee mtakatifu Simeoni alipomtabiria Maria kwamba upanga wa uchungu utaufuma moyo wake, akimaanisha mateso na kufa kwake Yesu Kristo mwanae.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Baba Yetu x 1
Salamu Maria x 7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA PILI (MT 2:12-18)
Katika uchungu wa pili tunakumbuka wakati Maria alipolazimika kukimbilia Misri kwasababu Herode katili alitaka kumuua mtoto Yesu.
Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu.
Baba Yetu x1
Salamu Maria x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA TATU (LK 2:41-51)
Katika uchungu wa tatu tunakumbuka wakati Maria alipompotezs mwanae mpendwa na kwa siku tatu akamtafuta kwa uchungu mpevu na machozi.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.
Baba Yetu x 1
Salamu Maria x7
Atukuzwe Baba
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA NNE (LK 23:26-31)
Katika uchungu wa nne tunakumbuka wakati Maria alipokutana na mwanae wa pekee akiwa amebeba msalaba akielekea mlima Kalvari ambako alikua akienda kusulubiwa kwa ajili ya wokovu wetu.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote.
Baba Yetu x1.
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA TANO (YOHN 19:25-27)
Katika uchungu wa tano tunakumbuka wakati Maria alipomwona mwanae Yesu ametundikwa juu ya msalaba na damu nyingi ikimwagika kutoka sehemu zote wa mwili wake.
Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria.
Baba Yetu x1
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA SITA (YHN 19:38-40)
Katika uchungu wa sita tunakumbuka wakati Maria alipomwona askari akimchoma mwanae ubavuni kwa mkuki na wakati mwili wa Yesu, baada ya kusgushwa msalabani, ulipolazwa mikononi mwake.
Tuombe neema ya kutotenda dhambi.
Baba Yetu x1
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA SABA (THN 19:40-41)
Katika uchungu wa saba tunakumbuka wakati Maria alipoona mwili wa mwanae wa pekee Yesu ukizikwa kaburini akitengana na mwanae ambaye kweli alimpenda mno.
Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria.
Baba Yetu x1.
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
TUOMBE:
Ee Bwana Mungu wetu, kwa njia ya mateso na kifo cha Mwokozi wetu Yesu Kristu na kwa masumbuko yaliyompata mama yake Bikira Maria, ulileta wokovu kwetu sisi wakosefu. Twakuomba utujalie huu wokovu, tupate kuacha njia za dhambi na kupata yote mema aliyotuahidia Yesu Kristo yeye anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu sasa na milele. Amina.
KUMBUKA
Kumbuka , Ee Bikira Maria, mwenye rehema, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba msaada wako, akitaka umuombee. Nami kwa matumaini hayo ninakukimbilia ee Mama Bikira mkuu wa Mabikira, ninakuja kwako, ninasimama mbele yako nikilalamika mimi mkosefu, Ee Mama wa Neno la Mungu, usikatae Maneno yangu, bali uyasikilize kwa wema na unitimizie. Amina.
Переглядів: 81

Відео

TAFAKARI YA DOMINIKA YA 23, MWAKA "B"- 08-09-2024
Переглядів 12920 годин тому
MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 08, 2024 DOMINIKA YA 23 YA MWAKA B WA KANISA MWANZO: Zab. 119:137, 124 Ee Bwana, wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili. Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako. SOMO 1 Isa. 35:4-7a Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Ndipo macho ya vipofu yatafum...
ROZARI YA BIKIRA MARIA MAMA WA MSAADA WA DAIMA
Переглядів 33719 годин тому
Pia huitwa ROZARI YA KASI, kwa uharaka wake wa kujibiwa mahitaji yetu. Sali kwa imani naye Mungu atakujalia yote kupitia kwa Mama yetu mpendwa sana Bikira Maria.
🔴 NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA - SIKU 12
Переглядів 32014 днів тому
Karibu kwenye Novena ya Mtakatifu Rita wa Kashia, mtetezi wa mambo yasiyowezekana. Katika siku hizi tisa za maombi na siku tatu za shukrani, tunajiunga pamoja kuomba miujiza, faraja, na nguvu kutoka kwa Mungu kupitia maombezi ya Mtakatifu Rita. Awe mwombezi wetu kwa Bwana katika changamoto tunazokabiliana nazo katika maisha yetu. Jiunge nasi katika tafakari hizi za kila siku na uwe na imani kwa...
🛑 WAFAHAMU MAASKOFU WOTE WA TANZANIA NA MAJIMBO YAO - 2024
Переглядів 21614 днів тому
Askofu Mkuu Damian Denis Dallu (Jimbo Kuu Katoliki la Songea) Kuzaliwa: 26 Apr 1955 (Kiponzelo) Upadri: 15 Nov 1984 (Geita) Uaskofu: 30 Jul 2000 (Geita) Uaskofu Mkuu: 18 May 2014 (Songea) Askofu Flavian Matindi Kassala (Jimbo Katoliki la Geita) Kuzaliwa: 4 Dec 1967 (Sumve) Upadri: 11 Jul 1999 (Geita) Uaskofu: 12 Jun 2016 (Geita) Askofu Thomas John Kiangio (Jimbo Katoliki la Tanga) Kuzaliwa: 17 ...
🛑 TAZAMA WATOTO WAKATOLIKI WALIVYOIMBA NA KUCHEZA VIZURI - PAROKIA YA KINYEREZI
Переглядів 2,4 тис.Місяць тому
WATOTO WENYE VIPAJI VYA KUIMBA NA KUCHEZA🙏🏾 MUNGU AWABARIKI KWA NYIMBO HIZI
Maandamano ya wafransiskani Jumapili ya Matawi
Переглядів 4445 місяців тому
JUMAPILI YA MATAWI _ St. Bonaventure University - Lusaka, Zambia@st.bonaventureuniversityza7385
Dominika ya Matawi | Mwanzo wa Juma Kuu | Maadhimisho ya Mafumbo ya Kanisa
Переглядів 5385 місяців тому
Na Padre Paschal Ighondo - Vatican
Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, yalivyoandikwa na Mt. Marko | Jumapili ya Matawi
Переглядів 3,5 тис.5 місяців тому
Jumapili ya Matawi • Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo kama yalivyoandikwa na Mt. Marko Kiongozi: Mara kulipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza zima. Wakamfunga Yesu, wakamchukua. Wakampeleka mbele ya Pilato. Pilato akamuuliza. Pilato: Wewe ndiye mfalme wa wayahudi? Kiongozi: Akajibu, akamwambia Yesu: Wewe wasema. Kiongozi: Nao wakuu wa makuha...
Dominika ya Tano ya kwaresma | Mahubiri
Переглядів 2775 місяців тому
Tafakari Dominika ya Tano ya Kwaresima Mwaka B: Agano Jipya Na La Milele SOMO LA KWANZA: Yeremia 31:31-34 Yeremia anawaambia watu kwamba Bwana atafanya agano jipya nao, akiweka sheria ndani ya mioyo yao. WIMBO WA KATIKATI: Zaburi 51:3-4,12-13,14-15 Maombi ya rehema na msamaha wa Mungu SOMO LA PILI: Waebrania 5:7-9 Kupitia mateso yake, Yesu alipata wokovu kwa wote wanaomtii. INJILI: Yohana 12:20...
Njia ya Msalaba | Wafransiskani
Переглядів 6565 місяців тому
St. Bonaventure University - Lusaka
Huu hapa Mchakato mzima wa kumpata Askofu wa Kanisa Katoliki | kumweka wakfu na mengineyo
Переглядів 4,9 тис.5 місяців тому
MCHAKATO MZIMA WA KUMPATA ASKOFU KATIKA KANISA KATOLIKI. Imeelezwa na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Marehemu Padre Raymond Saba
Dominika ya Nne ya Kwaresma | Mahubiri
Переглядів 2965 місяців тому
Tafakari Dominika ya Nne ya Kwaresima: Uzima wa Milele. Na Padre Paschal Ighondo - Vatican
Dominika ya Tatu ya Kwaresma | Mahubiri
Переглядів 5996 місяців тому
Dominika ya Tatu ya Kwaresima Mwaka B Somo la Kwanza: Kutoka 20: 1-17 Wimbo wa Katikati: Zaburi 19: 8, 9, 10, 11 Somo la Pili: 1 Wakorintho 1: 22-25 Injili: John 2: 13-25 Na Padre Paschal Ighondo, - Vatican.
Mungu wangu mbona umeniacha - wimbo wa Kwaresma
Переглядів 1,6 тис.6 місяців тому
Mungu wangu mbona umeniacha - wimbo wa Kwaresma
Dominika ya Pili ya Kwaresma | Mahubiri
Переглядів 1606 місяців тому
Dominika ya Pili ya Kwaresma | Mahubiri
Moyoni mwangu, nisiposema neno Asante - Franciscan Friars
Переглядів 1,7 тис.7 місяців тому
Moyoni mwangu, nisiposema neno Asante - Franciscan Friars
Bwana tunaleta Vipaji twakuomba sana pokea - Franciscan Friars
Переглядів 1,1 тис.7 місяців тому
Bwana tunaleta Vipaji twakuomba sana pokea - Franciscan Friars
Eyen Eron Abasi | Agnus Dei in Efik - Franciscan friars
Переглядів 8427 місяців тому
Eyen Eron Abasi | Agnus Dei in Efik - Franciscan friars
Kama Ayala - Franciscan Friars
Переглядів 1,5 тис.7 місяців тому
Kama Ayala - Franciscan Friars
Tazama Wafransiskani wakisherekea siku ya maisha ya waliowekwa wakfu
Переглядів 7927 місяців тому
Tazama Wafransiskani wakisherekea siku ya maisha ya waliowekwa wakfu
1 - 3 | NOVENA KWA MT. RITA WA KASHIA | NOVENA ISIYOSHINDWA KITU
Переглядів 16 тис.7 місяців тому
1 - 3 | NOVENA KWA MT. RITA WA KASHIA | NOVENA ISIYOSHINDWA KITU
TUMEMALIZA MWAKA SALAMA - Kwaya ya Mt. Donbosco na mt. Consolata - SUA Main Campus.
Переглядів 7898 місяців тому
TUMEMALIZA MWAKA SALAMA - Kwaya ya Mt. Donbosco na mt. Consolata - SUA Main Campus.
SALA YA ASUBUHI
Переглядів 3,6 тис.9 місяців тому
SALA YA ASUBUHI
HISTORIA FUPI YA MAISHA YA MT. RITA WA KASHIA | UMUHIMU WA KUSALI NOVENA YAKE
Переглядів 2,6 тис.9 місяців тому
HISTORIA FUPI YA MAISHA YA MT. RITA WA KASHIA | UMUHIMU WA KUSALI NOVENA YAKE
Kanisa kuu la Jimbo Katoliki la MBULU - Kanisa la kiaskofu
Переглядів 2,2 тис.9 місяців тому
Kanisa kuu la Jimbo Katoliki la MBULU - Kanisa la kiaskofu
Ndugu Wakapuchini - St Bonaventure university - Lusaka, Zambia
Переглядів 1,3 тис.10 місяців тому
Ndugu Wakapuchini - St Bonaventure university - Lusaka, Zambia
NOVENA YA MTAKATIFU PHILOMENA
Переглядів 47411 місяців тому
NOVENA YA MTAKATIFU PHILOMENA
NOVENA YA MT. ANTONI WA PADUA - Siku Tisa
Переглядів 8 тис.11 місяців тому
NOVENA YA MT. ANTONI WA PADUA - Siku Tisa
NOVENA YA MTAKATIFU PADRE PIO | siku tisa
Переглядів 1,2 тис.11 місяців тому
NOVENA YA MTAKATIFU PADRE PIO | siku tisa

КОМЕНТАРІ